Galatians 5
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Kristo alitupa uhuru akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa.Select Galatians 5:1
2Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.Select Galatians 5:2
3Nasema tena wazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika Sheria yote.Select Galatians 5:3
4Kama mnatazamia kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.Select Galatians 5:4
5Kwa upande wetu, lakini, sisi tunatumaini kwamba kwa nguvu ya Roho tunakubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani.Select Galatians 5:5
6Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.Select Galatians 5:6
7Mwenendo wenu ulikuwa mzuri! Nani, basi aliyewazuia kuuzingatia ukweli?Select Galatians 5:7
8Aliyesababisha hali hiyo si Mungu ambaye amewaiteni.Select Galatians 5:8
9"chachu kidogo tu huchachusha donge lote la unga!"Select Galatians 5:9
10Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba ninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni--awe nani au nani--hakika ataadhibiwa.Select Galatians 5:10
11Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.Select Galatians 5:11
12Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!Select Galatians 5:12
13Ninyi, ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo.Select Galatians 5:13
14Maana Sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: "Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."Select Galatians 5:14
15Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe!Select Galatians 5:15
16Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia.Select Galatians 5:16
17Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka ninyi wenyewe.Select Galatians 5:17
18Kama mkiongozwa na Roho, basi, hamko tena chini ya Sheria.Select Galatians 5:18
19Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati, ufisadi;Select Galatians 5:19
20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano;Select Galatians 5:20
21husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawatakuwa na nafasi yao katika ufalme wa Mungu.Select Galatians 5:21
22Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,Select Galatians 5:22
23upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.Select Galatians 5:23
24Wale walio wa Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.Select Galatians 5:24
25Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake.Select Galatians 5:25
26Basi, tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu.Select Galatians 5:26
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation