1 Corinthians 12
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya:Select 1 Corinthians 12:1
2Mnajua kwamba, kabla ya kuongoka kwenu, mlitawaliwa na kupotoshwa na sanamu tupu.Select 1 Corinthians 12:2
3Basi, jueni kwamba mtu yeyote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi kusema: "Yesu alaaniwe!" Hali kadhalika, mtu yeyote hawezi kusema: "Yesu ni Bwana," asipoongozwa na Roho Mtakatifu.Select 1 Corinthians 12:3
4Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja.Select 1 Corinthians 12:4
5Kuna namna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja.Select 1 Corinthians 12:5
6Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote.Select 1 Corinthians 12:6
7Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote.Select 1 Corinthians 12:7
8Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima, na mwingine ujumbe wa elimu apendavyo Roho huyohuyo.Select 1 Corinthians 12:8
9Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpa mwingine kipaji cha kuponya;Select 1 Corinthians 12:9
10humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua.Select 1 Corinthians 12:10
11Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.Select 1 Corinthians 12:11
12Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote--ingawaje ni vingi--hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.Select 1 Corinthians 12:12
13Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.Select 1 Corinthians 12:13
14Mwili hauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi.Select 1 Corinthians 12:14
15Kama mguu ungejisemea: "Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si mali ya mwili", je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha!Select 1 Corinthians 12:15
16Kama sikio lingejisemea: "Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili", je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!Select 1 Corinthians 12:16
17Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa?Select 1 Corinthians 12:17
18Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.Select 1 Corinthians 12:18
19Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?Select 1 Corinthians 12:19
20Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja.Select 1 Corinthians 12:20
21Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: "Sikuhitaji wewe", wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: "Siwahitaji ninyi."Select 1 Corinthians 12:21
22Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.Select 1 Corinthians 12:22
23Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,Select 1 Corinthians 12:23
24ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwa heshima,Select 1 Corinthians 12:24
25ili kusiweko na utengano katika mwili bali viungo vyote vishughulikiane.Select 1 Corinthians 12:25
26Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.Select 1 Corinthians 12:26
27Basi, ninyi nyote ni mwili wa Kristo; kila mmoja wenu ni kiungo cha mwili huo.Select 1 Corinthians 12:27
28Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.Select 1 Corinthians 12:28
29Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza?Select 1 Corinthians 12:29
30Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha?Select 1 Corinthians 12:30
31Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa nitawaonyesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote.Select 1 Corinthians 12:31
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation