1 Corinthians 15
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Sasa ndugu, napenda kuwakumbusha ile Habari Njema niliyowahubirieni nanyi mkaipokea na kusimama imara ndani yake.Select 1 Corinthians 15:1
2Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure.Select 1 Corinthians 15:2
3Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu;Select 1 Corinthians 15:3
4kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa;Select 1 Corinthians 15:4
5kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili.Select 1 Corinthians 15:5
6Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.Select 1 Corinthians 15:6
7Baadaye alimtokea Yakobo kisha akawatokea mitume wote.Select 1 Corinthians 15:7
8Baada ya wote, akanitokea hata mimi, mimi niliyekuwa kama mtu aliyezaliwa kabla ya wakati.Select 1 Corinthians 15:8
9Maana mimi ni mdogo kabisa miongoni mwa mitume na wala sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililidhulumu kanisa la Mungu.Select 1 Corinthians 15:9
10Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.Select 1 Corinthians 15:10
11Lakini hata hivyo, iwe wao ndio wahubirio au mimi nihubiriye, haidhuru, hiki ndicho tunachuhubiri, na hiki ndicho mnachoamini.Select 1 Corinthians 15:11
12Sasa, maadam inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?Select 1 Corinthians 15:12
13Kama hakuna ufufuo wa wafu, basi, Kristo naye hakufufuka;Select 1 Corinthians 15:13
14na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana.Select 1 Corinthians 15:14
15Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongo mbele ya Mungu, maana tulisema kwamba Mungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye hakumfufua--kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi.Select 1 Corinthians 15:15
16Maana, ikiwa ni kweli kwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristo hakufufuka.Select 1 Corinthians 15:16
17Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu.Select 1 Corinthians 15:17
18Zaidi ya hayo, wale wote waliokufa wakiwa wameungana na Kristo wamepotea kabisa.Select 1 Corinthians 15:18
19Kama matumaini yetu katika Kristo yanahusu tu maisha haya ya sasa, basi, sisi ni watu wa kusikitikiwa zaidi kuliko wengine wote duniani.Select 1 Corinthians 15:19
20Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, limbuko lao wale waliolala katika kifo.Select 1 Corinthians 15:20
21Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyo hivyo nako kufufuka kutoka wafu kumesababishwa na mtu mmoja.Select 1 Corinthians 15:21
22Kama vile watu wote wanavyokufa kwa kujiunga na Adamu, vivyo hivyo wote watafufuliwa kwa kuungana na Kristo.Select 1 Corinthians 15:22
23Lakini kila mmoja kwa mpango wake: Kristo kwanza, halafu wale walio wake Kristo wakati Kristo atakapokuja.Select 1 Corinthians 15:23
24Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba Utawala, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu.Select 1 Corinthians 15:24
25Maana Kristo sharti atawale mpaka Mungu atakapowashinda adui zake na kuwaweka chini ya miguu yake.Select 1 Corinthians 15:25
26Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo.Select 1 Corinthians 15:26
27Maana, Maandiko yasema: "Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake." Lakini, Maandiko yanaposema: "Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale" ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.Select 1 Corinthians 15:27
28Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya Utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya Utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.Select 1 Corinthians 15:28
29Kama hakuna ufufuo, je watu wale wanaobatizwa kwa ajili ya wafu wanatumainia kupata nini? Kama wafu hawafufuliwi, ya nini kubatizwa kwa ajili yao?Select 1 Corinthians 15:29
30Na sisi, ya nini kujitia hatarini kila saa?Select 1 Corinthians 15:30
31Ndugu, mimi nakikabili kifo kila siku! Fahari niliyo nayo juu yenu katika kuungana na Kristo Yesu Bwana wetu inanifanya nitangaze jambo hili.Select 1 Corinthians 15:31
32Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, "Tule na tunywe, maana kesho tutakufa."Select 1 Corinthians 15:32
33Msidanganyike! Urafiki mbaya huharibu tabia njema.Select 1 Corinthians 15:33
34Amkeni! Anzeni kuishi vema, na acheni kutenda dhambi. Baadhi yenu hawamjui Mungu kabisa. Hii nawaambieni, ni aibu kubwa kwenu!Select 1 Corinthians 15:34
35Lakini mtu anaweza kuuliza: "Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani wakati watakapokuja tena?"Select 1 Corinthians 15:35
36Hayo ni maswali ya kijinga! Ukipanda mbegu, isipokufa kwanza haitaota.Select 1 Corinthians 15:36
37Unachopanda ni mbegu tu, labda ya ngano au nafaka nyingine, na si mmea mzima ambao hutokea baadaye.Select 1 Corinthians 15:37
38Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutaka mwenyewe; kila mbegu hupata mwili wake wa pekee.Select 1 Corinthians 15:38
39Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili ya binadamu ni ya namna moja, ya wanyama ni ya namna nyingine, ya ndege ni ya namna nyingine na miili ya samaki pia ni ya namna nyingine.Select 1 Corinthians 15:39
40Iko miili ya mbinguni na miili ya duniani; uzuri wa miili ya mbinguni ni mwingine, na na uzuri wa miili ya duniani ni mwingine.Select 1 Corinthians 15:40
41Uko uzuri wa jua, wa mwezi na wa nyota; hata nyota nazo huhitilafiana kwa uzuri.Select 1 Corinthians 15:41
42Ndivyo ilivyo kuhusu ufufuo wa wafu. Kama vile mbegu, mwili huzikwa ardhini ukiwa katika hali ya kuharibika, lakini hufufuliwa katika hali ya kutoharibika.Select 1 Corinthians 15:42
43Huzikwa katika hali duni, hufufuliwa katika hali tukufu; huzikwa katika hali dhaifu, hufufuliwa ukiwa wenye nguvu.Select 1 Corinthians 15:43
44Unapozikwa ni mwili wa kawaida, unapofufuliwa ni mwili wa kiroho. Kuna mwili wa kawaida na kutakuwa na mwili wa kiroho.Select 1 Corinthians 15:44
45Maana Maandiko yasema: "Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe mwenye uhai;" lakini adamu wa mwisho ni Roho awapaye watu uzima.Select 1 Corinthians 15:45
46Lakini unaotangulia kuwako si ule mwili wa kiroho, ila ule mwili wa kawaida kisha ule mwili wa kiroho.Select 1 Corinthians 15:46
47Adamu wa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitoka ardhini; mtu wa pili alitoka mbinguni.Select 1 Corinthians 15:47
48Wote walio wa dunia wako kama huyo mtu aliyeumbwa kwa udongo; wale walio wa mbinguni wako kama yule aliyetoka mbinguni.Select 1 Corinthians 15:48
49Kama vile tulivyofanana na yule aliyeumbwa kwa udongo, vivyo hivyo tutafanana na huyohuyo aliyetoka mbinguni.Select 1 Corinthians 15:49
50Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki Ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika.Select 1 Corinthians 15:50
51Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwaSelect 1 Corinthians 15:51
52wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana mbiu itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa.Select 1 Corinthians 15:52
53Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa.Select 1 Corinthians 15:53
54Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: "Kifo kimeangamizwa ushindi umekamilika!"Select 1 Corinthians 15:54
55"Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?"Select 1 Corinthians 15:55
56Ukali wa kifo hutokana na dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika Sheria.Select 1 Corinthians 15:56
57Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.Select 1 Corinthians 15:57
58Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.Select 1 Corinthians 15:58
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation