Luke 4
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Yesu alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.Select Luke 4:1
2Huko alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo wote hakula chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa.Select Luke 4:2
3Ndipo Ibilisi akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate."Select Luke 4:3
4Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Mtu haishi kwa mkate tu."Select Luke 4:4
5Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,Select Luke 4:5
6"Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.Select Luke 4:6
7Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."Select Luke 4:7
8Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."Select Luke 4:8
9Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu, akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu,Select Luke 4:9
10kwa maana imeandikwa: Atawaamuru malaika wake wakulinde,Select Luke 4:10
11na tena, Watakuchukua mikononi mwao usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe."Select Luke 4:11
12Lakini Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Usimjaribu Bwana Mungu wako."Select Luke 4:12
13Ibilisi alipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.Select Luke 4:13
14Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.Select Luke 4:14
15Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote.Select Luke 4:15
16Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti.Select Luke 4:16
17Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa:Select Luke 4:17
18"Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,Select Luke 4:18
19na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana."Select Luke 4:19
20Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho.Select Luke 4:20
21Naye akaanza kuwaambia, "Andiko hili mlilosikia likisomwa, limetimia leo."Select Luke 4:21
22Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakanena, "Je, huyu si mwana wa Yosefu?"Select Luke 4:22
23Naye akawaambia, "Bila shaka mtaniambia msemo huu: Mganga jiponye mwenyewe, na pia mtasema: Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako."Select Luke 4:23
24Akaendelea kusema, "Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji chake.Select Luke 4:24
25Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.Select Luke 4:25
26Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni.Select Luke 4:26
27Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani, mwenyeji wa Siria."Select Luke 4:27
28Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana.Select Luke 4:28
29Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.Select Luke 4:29
30Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.Select Luke 4:30
31Kisha Yesu akashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa wa Galilaya, akawa anawafundisha watu siku ya Sabato.Select Luke 4:31
32Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha.Select Luke 4:32
33Na katika lile sunagogi kulikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na roho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wa kuziba masikio:Select Luke 4:33
34"We! Yesu wa Nazareti! Kwa nini unatuingilia? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni mjumbe Mtakatifu wa Mungu!"Select Luke 4:34
35Lakini Yesu akamkemea huyo pepo akisema: "Nyamaza! Mtoke mtu huyu!" Basi, huyo pepo baada ya kumwangusha yule mtu chini, akamtoka bila kumdhuru hata kidogo.Select Luke 4:35
36Watu wote wakashangaa, wakawa wanaambiana, "Hili ni jambo la ajabu, maana kwa uwezo na nguvu anawaamuru pepo wachafu watoke, nao wanatoka!"Select Luke 4:36
37Habari zake zikaenea mahali pote katika mkoa ule.Select Luke 4:37
38Yesu alitoka katika lile sunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa na homa kali; wakamwomba amponye.Select Luke 4:38
39Yesu akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Mara yule mama akainuka, akawatumikia.Select Luke 4:39
40Jua lilipokuwa linatua, wote waliokuwa na wagonjwa wao mbalimbali waliwaleta kwake; naye akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao, akawaponya wote.Select Luke 4:40
41Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: "Wewe u Mwana wa Mungu!" Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo.Select Luke 4:41
42Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.Select Luke 4:42
43Lakini yeye akawaambia, "Ninapaswa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, maana nilitumwa kwa ajili hiyo."Select Luke 4:43
44Akawa anahubiri katika masunagogi ya Yudea.Select Luke 4:44
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation