Mark 3
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza.Select Mark 3:1
2Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki.Select Mark 3:2
3Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, "Njoo hapa katikati."Select Mark 3:3
4Kisha, akawauliza, "Je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuua?" Lakini wao hawakusema neno.Select Mark 3:4
5Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia huyo mtu, "Nyosha mkono wako!" Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.Select Mark 3:5
6Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wa kikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu.Select Mark 3:6
7Yesu aliondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaenda kando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea,Select Mark 3:7
8Idumea, ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.Select Mark 3:8
9Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.Select Mark 3:9
10Alikuwa amewaponya watu wengi, na wagonjwa wote wakawa wanamsonga ili wapate kumgusa.Select Mark 3:10
11Na watu waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake na kupaaza sauti, "Wewe ni Mwana wa Mungu!"Select Mark 3:11
12Lakini Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu.Select Mark 3:12
13Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea,Select Mark 3:13
14naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiriSelect Mark 3:14
15na wawe na mamlaka ya kuwafukuza pepo.Select Mark 3:15
16Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro),Select Mark 3:16
17Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake "wanangurumo"),Select Mark 3:17
18Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani naSelect Mark 3:18
19Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.Select Mark 3:19
20Kisha Yesu alikwenda nyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula.Select Mark 3:20
21Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo wakatoka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasema kwamba amepatwa na wazimu.Select Mark 3:21
22Nao walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, "Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo."Select Mark 3:22
23Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwa mifano, "Shetani anawezaje kumfukuza Shetani?Select Mark 3:23
24Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopigana, utawala huo hauwezi kudumu.Select Mark 3:24
25Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia.Select Mark 3:25
26Ikiwa basi, utawala wa Shetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu, bali utaangamia kabisa.Select Mark 3:26
27"Hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake, isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kumnyang'anya mali yake.Select Mark 3:27
28"Kweli nawaambieni, watu watasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote;Select Mark 3:28
29lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele."Select Mark 3:29
30(Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema, "Ana pepo mchafu.")Select Mark 3:30
31Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekea ujumbe kutaka kumwona.Select Mark 3:31
32Umati wa watu ulikuwa umekaa hapo kumzunguka. Basi, wakamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona."Select Mark 3:32
33Yesu akawaambia, "Mama yangu na ndugu zangu ni kina nani?"Select Mark 3:33
34Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema, "Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu.Select Mark 3:34
35Mtu yeyote anayefanya anayotaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu."Select Mark 3:35
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation