Matthew 14
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu.Select Matthew 14:1
2Basi, akawaambia watumishi wake, "Mtu huyu ni Yohane mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake."Select Matthew 14:2
3Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake. Sababu hasa niSelect Matthew 14:3
4kwamba alikuwa amemwambia Herode, "Si halali kwako kuishi na huyo mwanamke!"Select Matthew 14:4
5Herode alitaka kumwua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii.Select Matthew 14:5
6Katika sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa,Select Matthew 14:6
7hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyo msichana chochote atakachoomba.Select Matthew 14:7
8Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, "Nipe papahapa katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji."Select Matthew 14:8
9Mfalme alihuzunika, lakini kwa sababu ya kile kiapo chake na kwa sababu ya wale wageni karamuni, akaamuru apewe.Select Matthew 14:9
10Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane.Select Matthew 14:10
11Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake.Select Matthew 14:11
12Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.Select Matthew 14:12
13Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini.Select Matthew 14:13
14Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.Select Matthew 14:14
15Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula."Select Matthew 14:15
16Yesu akawaambia, "Si lazima waende, wapeni ninyi chakula."Select Matthew 14:16
17Lakini wao wakamwambia, "Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili."Select Matthew 14:17
18Yesu akawaambia, "Nileteeni hapa."Select Matthew 14:18
19Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.Select Matthew 14:19
20Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.Select Matthew 14:20
21Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto.Select Matthew 14:21
22Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ng'ambo ya ziwa wakati yeye anawaaga watu.Select Matthew 14:22
23Baada ya kuwaaga, alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwa jioni, yeye alikuwa huko peke yake,Select Matthew 14:23
24na wakati huo ile mashua ilikwishafika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikuwa inakwenda mrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.Select Matthew 14:24
25Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji.Select Matthew 14:25
26Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema, "Ni mzimu!" Wakapiga kelele kwa hofu.Select Matthew 14:26
27Mara, Yesu akasema nao, "Tulieni, ni mimi. Msiogope!"Select Matthew 14:27
28Petro akamwambia, "Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako."Select Matthew 14:28
29Yesu akasema, "Haya, njoo." Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.Select Matthew 14:29
30Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, "Bwana, niokoe!"Select Matthew 14:30
31Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, "Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?"Select Matthew 14:31
32Basi, wakapanda mashuani, na upepo ukatulia.Select Matthew 14:32
33Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, "Hakika wewe ni Mwana wa Mungu."Select Matthew 14:33
34Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti.Select Matthew 14:34
35Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote,Select Matthew 14:35
36wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake; wote waliomgusa walipona.Select Matthew 14:36
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation