Matthew 15
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Kisha Mafarisayo na walimu wa Sheria wakafika kutoka Yerusalemu, wakamwendea Yesu, wakamwuliza,Select Matthew 15:1
2"Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kutoka kwa wazee wetu? Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla ya kula!"Select Matthew 15:2
3Yesu akawajibu, "Kwa nini nanyi mnapendelea mapokeo yenu wenyewe na hamuijali Sheria ya Mungu?Select Matthew 15:3
4Mungu amesema: Waheshimu baba yako na mama yako, na Anayemkashifu baba yake au mama yake, lazima auawe.Select Matthew 15:4
5Lakini ninyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema: Kitu hiki nimemtolea Mungu,Select Matthew 15:5
6basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe.Select Matthew 15:6
7Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:Select Matthew 15:7
8Watu hawa, asema Mungu, huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.Select Matthew 15:8
9Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu."Select Matthew 15:9
10Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, "Sikilizeni na muelewe!Select Matthew 15:10
11Kitu kinachomtia mtu najisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu najisi."Select Matthew 15:11
12Kisha wanafunzi wakamwendea, wakamwambia, "Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa waliposikia maneno yako?"Select Matthew 15:12
13Lakini yeye akawajibu, "Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakuupanda, utang'olewa.Select Matthew 15:13
14Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni."Select Matthew 15:14
15Petro akadakia, "Tufafanulie huo mfano."Select Matthew 15:15
16Yesu akasema, "Hata nyinyi hamwelewi?Select Matthew 15:16
17Je, hamwelewi kwamba kila kinachoingia kinywani huenda tumboni na baadaye hutupwa nje chooni?Select Matthew 15:17
18Lakini yale yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi.Select Matthew 15:18
19Maana moyoni hutoka mawazo maovu yanayosababisha uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa.Select Matthew 15:19
20Hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi. Lakini kula chakula bila kunawa mikono hakumtii mtu najisi."Select Matthew 15:20
21Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na Sidoni.Select Matthew 15:21
22Basi, mama mmoja Mkaanani wa nchi hiyo alimjia, akapaaza sauti: "Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo."Select Matthew 15:22
23Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi, wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, "Mwambie aende zake kwa maana anatufuatafuata akipiga kelele."Select Matthew 15:23
24Yesu akajibu, "Sikutumwa ila kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo."Select Matthew 15:24
25Hapo huyo mama akaja, akapiga magoti mbele yake, akasema, "Mheshimiwa, nisaidie."Select Matthew 15:25
26Yesu akamjibu, "Si sawa kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."Select Matthew 15:26
27Huyo mama akajibu, "Ni kweli, Mheshimiwa; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao."Select Matthew 15:27
28Hapo Yesu akamjibu, "Mama, imani yako ni kubwa; basi, ufanyiwe kama unavyotaka." Yule binti yake akapona tangu saa hiyo wakati huohuo.Select Matthew 15:28
29Yesu alitoka hapo akaenda kando ya ziwa Galilaya, akapanda mlimani, akaketi.Select Matthew 15:29
30Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.Select Matthew 15:30
31Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea, waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; wakamsifu Mungu wa Israeli.Select Matthew 15:31
32Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, "Nawaonea watu hawa huruma kwa sababu kwa siku tatu wamekuwa nami, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende bila kula wasije wakazimia njiani."Select Matthew 15:32
33Wanafunzi wakamwambia, "Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?"Select Matthew 15:33
34Yesu akawauliza, "Mnayo mikate mingapi?" Wakamjibu, "Saba na visamaki vichache."Select Matthew 15:34
35Basi, Yesu akawaamuru watu wakae chini.Select Matthew 15:35
36Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.Select Matthew 15:36
37Wote wakala, wakashiba. Kisha wakakusanya makombo, wakajaza vikapu saba.Select Matthew 15:37
38Hao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto.Select Matthew 15:38
39Basi, Yesu akawaaga watu, akapanda mashua, akaenda katika eneo la Magadani.Select Matthew 15:39
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation