Skip to content
Church.wiki
Matthew

Matthew 22

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano:Select Matthew 22:1

2"Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.Select Matthew 22:2

3Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika.Select Matthew 22:3

4Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.Select Matthew 22:4

5Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake,Select Matthew 22:5

6na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua.Select Matthew 22:6

7Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.Select Matthew 22:7

8Kisha akawaambia watumishi wake: Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.Select Matthew 22:8

9Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje arusini.Select Matthew 22:9

10Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote, wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.Select Matthew 22:10

11"Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye hakuvaa mavazi ya arusi.Select Matthew 22:11

12Mfalme akamwuliza, Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la arusi? Lakini yeye akakaa kimya.Select Matthew 22:12

13Hapo mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno."Select Matthew 22:13

14Yesu akamaliza kwa kusema, "Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa."Select Matthew 22:14

15Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake.Select Matthew 22:15

16Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.Select Matthew 22:16

17Haya, twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa Kaisari?"Select Matthew 22:17

18Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, "EnyiSelect Matthew 22:18

19Nionyesheni fedha ya kulipia kodi." Nao wakamtolea sarafu ya fedha. sarafu ya fedha.Select Matthew 22:19

20Basi, Yesu akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya nani?"Select Matthew 22:20

21Wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Hapo Yesu akawaambia, "Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu."Select Matthew 22:21

22Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.Select Matthew 22:22

23Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. Hao ndio wale wasemao kwamba wafu hawafufuki.Select Matthew 22:23

24Basi, wakamwambia, "Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu yake watoto.Select Matthew 22:24

25Sasa, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa kisha akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane.Select Matthew 22:25

26Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa saba.Select Matthew 22:26

27Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama.Select Matthew 22:27

28Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba? Maana Wote saba walimwoa."Select Matthew 22:28

29Yesu akawajibu, "Kweli mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu!Select Matthew 22:29

30Maana wafu watakapofufuliwa hawataoa wala kuolewa, watakuwa kama malaika mbinguni.Select Matthew 22:30

31Lakini kuhusu suala la wafu kufufuka, hamjasoma yale aliyowaambieni Mungu?Select Matthew 22:31

32Aliwaambia, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo! Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."Select Matthew 22:32

33Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.Select Matthew 22:33

34Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja.Select Matthew 22:34

35Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu,Select Matthew 22:35

36"Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya Mose?"Select Matthew 22:36

37Yesu akamjibu, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote.Select Matthew 22:37

38Hii ndiyo amri kuu ya kwanza.Select Matthew 22:38

39Ya pili inafanana na hiyo: Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.Select Matthew 22:39

40Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili."Select Matthew 22:40

41Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu aliwauliza,Select Matthew 22:41

42"Ninyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?" Wakamjibu, "Wa Daudi."Select Matthew 22:42

43Yesu akawaambia, "Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema:Select Matthew 22:43

44Bwana alimwambia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.Select Matthew 22:44

45Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo Bwana, anawezaje kuwa mwanawe?"Select Matthew 22:45

46Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.Select Matthew 22:46

Next: Matthew 23Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Matthew

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.