Skip to content
Church.wiki
Matthew

Matthew 25

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1"Wakati huo, Ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi.Select Matthew 25:1

2Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.Select Matthew 25:2

3Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.Select Matthew 25:3

4Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.Select Matthew 25:4

5Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wanawali wote wote walisinzia, wakalala.Select Matthew 25:5

6Usiku wa manane kukawa na kelele: Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.Select Matthew 25:6

7Hapo wale wanawali wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.Select Matthew 25:7

8Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.Select Matthew 25:8

9Lakini wale wenye busara wakawaambia, Hayatatutosha sisi na ninyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!Select Matthew 25:9

10Basi, wale wanawali wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana arusi akafika, na wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la arusi, kisha mlango ukafungwa.Select Matthew 25:10

11Baadaye wale wanawali wengine wakaja, wakaita: Bwana, bwana, tufungulie!Select Matthew 25:11

12Lakini yeye akawajibu, Nawaambieni kweli, siwajui ninyi."Select Matthew 25:12

13Kisha Yesu akasema, "Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.Select Matthew 25:13

14"Itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ng'ambo: aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake.Select Matthew 25:14

15Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake: mmoja sarafu tano za fedha ziitwazo talanta, mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja, kisha akasafiri.Select Matthew 25:15

16Mara yule aliyekabidhiwa talanta tano akafanya kazi nazo akapata faida talanta tano.Select Matthew 25:16

17Hali kadhalika na yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapata faida talanta mbili.Select Matthew 25:17

18Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaenda akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake.Select Matthew 25:18

19"Baada ya muda mrefu, yule bwana alirudi, akaanza kukagua hesabu ya matumizi na mapato ya fedha yake.Select Matthew 25:19

20Mtumishi aliyekabidhiwa talanta tano akaja amechukua zile talanta tano faida, akamwambia, Bwana, ulinikabidhi talanta tano, hapa pana talanta tano zaidi faida niliyopata.Select Matthew 25:20

21Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.Select Matthew 25:21

22"Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida, akisema, Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata.Select Matthew 25:22

23Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.Select Matthew 25:23

24"Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaja, akasema, Bwana, najua wewe ni mtu mgumu; wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na kukusanya pale ambapo hukutawanya.Select Matthew 25:24

25Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali yako.Select Matthew 25:25

26"Bwana wake akamwambia, Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.Select Matthew 25:26

27Ilikupasa basi, kuiweka fedha yangu katika benki, nami ningelichukua mtaji wangu na faida yake!Select Matthew 25:27

28Basi, mnyang'anyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi.Select Matthew 25:28

29Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.Select Matthew 25:29

30Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani! Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.Select Matthew 25:30

31"Wakati Mwana wa Mtu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu ya kiti chake cha enzi kitukufu,Select Matthew 25:31

32na mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.Select Matthew 25:32

33Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa kushoto.Select Matthew 25:33

34"Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni Ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.Select Matthew 25:34

35Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;Select Matthew 25:35

36nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.Select Matthew 25:36

37Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji?Select Matthew 25:37

38Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika?Select Matthew 25:38

39Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?Select Matthew 25:39

40Mfalme atawajibu, Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.Select Matthew 25:40

41"Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.Select Matthew 25:41

42Maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji.Select Matthew 25:42

43Nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa na mfungwa nanyi hamkuja kunitazama.Select Matthew 25:43

44"Hapo nao watajibu, Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, ukiwa mgeni au bila nguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasi hatukuja kukuhudumia?Select Matthew 25:44

45Naye atawajibu, Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.Select Matthew 25:45

46Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale waadilifu watakwenda kwenye uzima wa milele."Select Matthew 25:46

Next: Matthew 26Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Matthew

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.