Ephesians 6
Swahili
Translation: SWAHILI
1Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.Select Ephesians 6:1
2"Waheshimu Baba na mama yako," hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,Select Ephesians 6:2
3"Upate fanaka na miaka mingi duniani."Select Ephesians 6:3
4Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.Select Ephesians 6:4
5Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.Select Ephesians 6:5
6Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi ni watumishi wa Kristo.Select Ephesians 6:6
7Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.Select Ephesians 6:7
8Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.Select Ephesians 6:8
9Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, kwake cheo cha mtu si kitu.Select Ephesians 6:9
10Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu.Select Ephesians 6:10
11Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.Select Ephesians 6:11
12Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.Select Ephesians 6:12
13Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti.Select Ephesians 6:13
14Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani,Select Ephesians 6:14
15na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.Select Ephesians 6:15
16Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu.Select Ephesians 6:16
17Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.Select Ephesians 6:17
18Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.Select Ephesians 6:18
19Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti.Select Ephesians 6:19
20Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.Select Ephesians 6:20
21Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.Select Ephesians 6:21
22Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo.Select Ephesians 6:22
23Ninawatakieni ninyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.Select Ephesians 6:23
24Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho.Select Ephesians 6:24
Swahili (SWAHILI) · Public Domain