John 10
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Yesu alisema "Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi.Select John 10:1
2Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo.Select John 10:2
3Mngoja mlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake na kuwaongoza nje.Select John 10:3
4Akisha watoa nje huwatangulia mbele nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.Select John 10:4
5Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake."Select John 10:5
6Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.Select John 10:6
7Basi, akasema tena, "Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.Select John 10:7
8Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza.Select John 10:8
9Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho.Select John 10:9
10Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima--uzima kamili.Select John 10:10
11"Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.Select John 10:11
12Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.Select John 10:12
13Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.Select John 10:13
14Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,Select John 10:14
15kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.Select John 10:15
16Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.Select John 10:16
17"Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.Select John 10:17
18Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye."Select John 10:18
19Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.Select John 10:19
20Wengi wao wakasema, "Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?"Select John 10:20
21Wengine wakasema, "Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?"Select John 10:21
22Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya Kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.Select John 10:22
23Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.Select John 10:23
24Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, "Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi."Select John 10:24
25Yesu akawajibu, "Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.Select John 10:25
26Lakini ninyi hamsadiki kwa sababu ninyi si kondoo wangu.Select John 10:26
27Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata.Select John 10:27
28Mimi nawapa uzima wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu.Select John 10:28
29Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wale hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba.Select John 10:29
30Mimi na Baba, tu mmoja."Select John 10:30
31Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie.Select John 10:31
32Yesu akawaambia, "Nimewaonyesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?"Select John 10:32
33Wayahudi wakamjibu, "Hatukupigi mawe kwa ajili ya tendo jema, ila kwa sababu ya kukufuru! Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe ni binadamu tu."Select John 10:33
34Yesu akawajibu, "Je, haikuandikwa katika Sheria yenu: Mimi nimesema, ninyi ni miungu?Select John 10:34
35Mungu aliwaita miungu wale waliopewa neno lake; nasi twajua kwamba Maandiko Matakatifu yasema ukweli daima.Select John 10:35
36Je, yeye ambaye Baba alimweka wakfu na kumtuma ulimwenguni, mnamwambia: Unakufuru, eti kwa sababu nilisema: Mimi ni Mwana wa Mungu?Select John 10:36
37Kama sifanyi kazi za Baba yangu msiniamini.Select John 10:37
38Lakini ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, walau ziaminini hizo kazi mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake."Select John 10:38
39Wakajaribu tena kumkamata lakini akachopoka mikononi mwao.Select John 10:39
40Yesu akaenda tena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.Select John 10:40
41Watu wengi walimwendea wakasema, "Yohane hakufanya ishara yoyote. Lakini yale yote Yohane aliyosema juu ya mtu huyu ni kweli kabisa."Select John 10:41
42Watu wengi mahali hapo wakamwamini.Select John 10:42
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation