John 11
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa mahali walipokaa Maria na Martha, dada yake.Select John 11:1
2Maria ndiye yule aliyempaka Bwana marashi na kumpangusa kwa nywele zake. Lazaro, kaka yake, ndiye aliyekuwa mgonjwa.)Select John 11:2
3Basi, hao dada wakatuma ujumbe huu kwa Yesu: "Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!"Select John 11:3
4Yesu aliposikia hivyo akasema, "Ugonjwa huo hautaleta kifo, ila ni kwa ajili ya kumtukuza Mungu; ameugua ili kwa njia hiyo Mwana wa Mungu atukuzwe."Select John 11:4
5Yesu aliwapenda Martha, dada yake na Lazaro.Select John 11:5
6Alipopata habari kwamba Lazaro ni mgonjwa, Yesu aliendelea kukaa mahali hapo alipokuwa kwa siku mbili zaidi.Select John 11:6
7Kisha akawaambia wanafunzi wake, "Twendeni tena Yudea!"Select John 11:7
8Wanafunzi wakamwambia, "Mwalimu! Muda mfupi tu umepita tangu Wayahudi walipotaka kukuua kwa mawe, nawe unataka kwenda huko tena?"Select John 11:8
9Yesu akajibu, "Je, saa za mchana si kumi na mbili? Basi, mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa kuwa anauona mwanga wa ulimwengu huu.Select John 11:9
10Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maana mwanga haumo ndani yake."Select John 11:10
11Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, akawaambia, "Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini mimi nitakwenda kumwamsha."Select John 11:11
12Wanafunzi wake wakamwambia, "Bwana, ikiwa amelala, basi atapona."Select John 11:12
13Wao walidhani kwamba alikuwa amesema juu ya kulala usingizi, kumbe alikuwa amesema juu ya kifo cha Lazaro.Select John 11:13
14Basi, Yesu akawaambia waziwazi, "Lazaro amekufa;Select John 11:14
15Lakini nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini. Haya, twendeni kwake."Select John 11:15
16Thoma (aitwaye Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, "Twendeni nasi tukafe pamoja naye!"Select John 11:16
17Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne.Select John 11:17
18Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu umbali upatao kilomita tatu.Select John 11:18
19Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao.Select John 11:19
20Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani.Select John 11:20
21Martha akamwambia Yesu, "Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!Select John 11:21
22Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa."Select John 11:22
23Yesu akamwambia, "Kaka yako atafufuka."Select John 11:23
24Martha akamjibu, "Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho."Select John 11:24
25Yesu akamwambia, "Mimi ndimi ufufuo na uzima. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi:Select John 11:25
26na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?"Select John 11:26
27Martha akamwambia, "Ndiyo Bwana! Naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni."Select John 11:27
28Baada ya kusema hayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwabia faraghani, "Mwalimu yuko hapa, anakuita."Select John 11:28
29Naye aliposikia hivyo, akainuka mara, akamwendea Yesu.Select John 11:29
30Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado mahali palepale Martha alipomlaki.Select John 11:30
31Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.Select John 11:31
32Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwabia, "Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!"Select John 11:32
33Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni.Select John 11:33
34Kisha akawauliza, "Mlimweka wapi?" Wakamwambia, "Bwana, njoo uone."Select John 11:34
35Yesu akalia machozi.Select John 11:35
36Basi, Wayahudi wakasema, "Tazameni jinsi alivyompenda!"Select John 11:36
37Lakini baadhi yao wakasema, "Je, huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya Lazaro asife?"Select John 11:37
38Basi, Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni, akafika kaburini. Kaburi lenyewe lilikuwa pango, na lilikuwa limefunikwa kwa jiwe.Select John 11:38
39Yesu akasema, "Ondoeni hilo jiwe!" Martha, dada yake huyo aliyekufa, akamwambia, "Bwana, amekwishaanza kunuka; amekaa kaburini siku nne!"Select John 11:39
40Yesu akamwambia, "Je, sikukwambia kwamba ukiamini utaona utukufu wa Mungu?"Select John 11:40
41Basi, wakaliondoa lile jiwe. Yesu akatazama juu mbinguni, akasema, "Nakushukuru Baba kwa kuwa wewe wanisikiliza.Select John 11:41
42Najua kwamba unanisikiliza daima. Lakini nimesema hayo kwa ajili ya watu hawa waliopo hapa ili wapate kuamini kwamba wewe ndiwe uliyenituma."Select John 11:42
43Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: "Lazaro! Toka nje!"Select John 11:43
44Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, "Mfungueni, mkamwache aende zake."Select John 11:44
45Basi, Wayahudi wengi waliokuwa wamefika kwa Maria walipoona kitendo hicho alichokifanya Yesu wakamwamini.Select John 11:45
46Lakini baadhi yao walikwenda kwa Mafarisayo wakatoa taarifa ya jambo hilo alilofanya Yesu.Select John 11:46
47kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza kuu, wakasema, "Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.Select John 11:47
48Tukimwacha tu watu wote watamwamini, nao Waroma watakuja kuliharibu Hekalu letu na taifa letu!"Select John 11:48
49Hapo, mmoja wao aitwaye Kayafa, ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, akawaambia, "Ninyi hamjui kitu!Select John 11:49
50Je, hamwoni kwamba ni afadhali kwenu mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa zima liangamizwe?"Select John 11:50
51Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, alibashiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao;Select John 11:51
52na wala si kwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watoto wa Mungu waliotawanyika.Select John 11:52
53Basi, tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi walifanya mipango ya kumwua Yesu.Select John 11:53
54Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati ya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.Select John 11:54
55Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa karibu, na watu wengi walikwenda Yerusalemu ili wajitakase kabla ya sikukuu hiyo.Select John 11:55
56Basi, wakawa wanamtafuta Yesu; nao walipokusanyika pamoja Hekaluni wakaulizana, "Mwaonaje? Yaonekana kwamba haji kabisa kwenye sikukuu, au sivyo?"Select John 11:56
57Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba mtu akijua mahali aliko Yesu awaarifu kusudi wamtie nguvuni.Select John 11:57
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation