John 15
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1"Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.Select John 15:1
2Yeye huliondoa ndani yangu kila tawi lisilozaa matunda, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.Select John 15:2
3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya ule ujumbe niliowaambieni.Select John 15:3
4Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Tawi haliwezi peke yake kuzaa matunda lisipokaa katika mzabibu hali kadhalika nanyi hamwezi kuzaa matunda msipokaa ndani yangu.Select John 15:4
5"Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi yake. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo atazaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.Select John 15:5
6Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue.Select John 15:6
7Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.Select John 15:7
8Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.Select John 15:8
9Mimi nimewapenda ninyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu.Select John 15:9
10Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.Select John 15:10
11Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike.Select John 15:11
12Hii ndiyo amri yangu: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda ninyi.Select John 15:12
13Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.Select John 15:13
14Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru.Select John 15:14
15Ninyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita ninyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu.Select John 15:15
16Ninyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapa ninyi chochote mumwombacho kwa jina langu.Select John 15:16
17Basi, amri yangu kwenu ndiyo hii: pendaneni.Select John 15:17
18"Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.Select John 15:18
19Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda ninyi kama watu wake. Lakini kwa vile ninyi si wa ulimwengu, ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni.Select John 15:19
20Kumbukeni niliyowaambieni: mtumishi si mkuu zaidi kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia.Select John 15:20
21Lakini hayo yote watawatendeeni ninyi kwa sababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye aliyenituma.Select John 15:21
22Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi.Select John 15:22
23Anayenichukia mimi, anamchukia na Baba yangu pia.Select John 15:23
24Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakinichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia.Select John 15:24
25Na hivi ni lazima yatimie yale yaliyoandikwa katika Sheria yao: Wamenichukia bure!Select John 15:25
26"Atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi.Select John 15:26
27Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo.Select John 15:27
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation