Skip to content
Church.wiki
1 Corinthians

1 Corinthians 10

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari.Select 1 Corinthians 10:1

2Wote walibatizwa katika umoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari.Select 1 Corinthians 10:2

3Wote walikula chakula kilekile cha kiroho,Select 1 Corinthians 10:3

4wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.Select 1 Corinthians 10:4

5Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.Select 1 Corinthians 10:5

6Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.Select 1 Corinthians 10:6

7Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: "Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza."Select 1 Corinthians 10:7

8Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu ishirini na tatu elfu.Select 1 Corinthians 10:8

9Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.Select 1 Corinthians 10:9

10Wala msinung'unike kama baadhi yao walivyonung'unika, wakaangamizwa na Mwangamizi!Select 1 Corinthians 10:10

11Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwisho wa nyakati unatukabili.Select 1 Corinthians 10:11

12Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.Select 1 Corinthians 10:12

13Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.Select 1 Corinthians 10:13

14Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu.Select 1 Corinthians 10:14

15Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo.Select 1 Corinthians 10:15

16Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?Select 1 Corinthians 10:16

17Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.Select 1 Corinthians 10:17

18Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe: kwao, wenye kula vilivyotambikiwa madhabahuni waliungana na hiyo madhabahu.Select 1 Corinthians 10:18

19Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya sanamu?Select 1 Corinthians 10:19

20Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe na ushirika na pepo.Select 1 Corinthians 10:20

21Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya pepo.Select 1 Corinthians 10:21

22Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu zaidi kuliko yeye?Select 1 Corinthians 10:22

23Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga.Select 1 Corinthians 10:23

24Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake.Select 1 Corinthians 10:24

25Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu;Select 1 Corinthians 10:25

26maana Maandiko yasema: "Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana."Select 1 Corinthians 10:26

27Kama mtu ambaye si muumini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.Select 1 Corinthians 10:27

28Lakini mtu akiwaambieni: "Chakula hiki kimetambikiwa sanamu," basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.Select 1 Corinthians 10:28

29Nasema, "kwa ajili ya dhamiri," si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: "Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?Select 1 Corinthians 10:29

30Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?"Select 1 Corinthians 10:30

31Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.Select 1 Corinthians 10:31

32Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu.Select 1 Corinthians 10:32

33Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.Select 1 Corinthians 10:33

Next: 1 Corinthians 11Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

1 Corinthians

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.