Skip to content
Church.wiki
1 Corinthians

1 Corinthians 13

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.Select 1 Corinthians 13:1

2Tena, naweza kuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, nikafahamu siri zote na kujua kila kitu; naweza kuwa na imani yote hata nikaweza kuihamisha milima, lakini kama sina upendo mimi si kitu.Select 1 Corinthians 13:2

3Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.Select 1 Corinthians 13:3

4Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.Select 1 Corinthians 13:4

5Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya,Select 1 Corinthians 13:5

6hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.Select 1 Corinthians 13:6

7Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.Select 1 Corinthians 13:7

8Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.Select 1 Corinthians 13:8

9Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili.Select 1 Corinthians 13:9

10Lakini kile kilicho kikamilifu kitakapofika, vyote visivyo vikamilifu vitatoweka.Select 1 Corinthians 13:10

11Nilipokuwa mtoto mchanga nilisema kitoto, nilifahamu kitoto, nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtu mzima, mambo ya kitoto nimeyaacha.Select 1 Corinthians 13:11

12Tunachoona sasa ni kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapo baadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapo baadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua mimi.Select 1 Corinthians 13:12

13Sasa yanadumu haya matatu: imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.Select 1 Corinthians 13:13

Next: 1 Corinthians 14Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

1 Corinthians

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.