Skip to content
Church.wiki
1 Corinthians

1 Corinthians 16

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.Select 1 Corinthians 16:1

2Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja.Select 1 Corinthians 16:2

3Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.Select 1 Corinthians 16:3

4Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami.Select 1 Corinthians 16:4

5Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia--maana nataraji kupitia Makedonia.Select 1 Corinthians 16:5

6Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.Select 1 Corinthians 16:6

7Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.Select 1 Corinthians 16:7

8Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste.Select 1 Corinthians 16:8

9Mlango uko wazi kabisa kwa ajili ya kazi yangu muhimu hapa, ingawa wapinzani nao ni wengi.Select 1 Corinthians 16:9

10Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.Select 1 Corinthians 16:10

11Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieni aendelee na safari yake kwa amani ili aweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamoja na ndugu zetu.Select 1 Corinthians 16:11

12Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.Select 1 Corinthians 16:12

13Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu.Select 1 Corinthians 16:13

14Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo.Select 1 Corinthians 16:14

15Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu. Ninawasihi ninyi ndugu zangu,Select 1 Corinthians 16:15

16muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumikia pamoja nao.Select 1 Corinthians 16:16

17Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunato na Akaiko wamefika; wamelijaza pengo lililokuwako kwa kutokuwako kwenu.Select 1 Corinthians 16:17

18Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwa hiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namna hii.Select 1 Corinthians 16:18

19Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priskila pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika Bwana.Select 1 Corinthians 16:19

20Ndugu wote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa ishara ya mapendo ya Mungu.Select 1 Corinthians 16:20

21Mimi Paulo nawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe.Select 1 Corinthians 16:21

22Yeyote asiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANA THA--BWANA, njoo!Select 1 Corinthians 16:22

23Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.Select 1 Corinthians 16:23

24Mapendo yangu yawe kwenu katika kuungana na Kristo Yesu.Select 1 Corinthians 16:24

Next: 2 Corinthians 1Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

1 Corinthians

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.