Skip to content
Church.wiki
Galatians

Galatians 6

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Ndugu, kama mkimwona mtu fulani amekosea, basi, ninyi mnaoongozwa na Roho mwonyeni mtu huyo ajirekebishe; lakini fanyeni hivyo kwa upole, mkiwa na tahadhari msije nanyi wenyewe mkajaribiwa.Select Galatians 6:1

2Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo.Select Galatians 6:2

3Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya mwenyewe.Select Galatians 6:3

4Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine.Select Galatians 6:4

5Maana kila mmoja anao mzigo wake mwenyewe wa kubeba.Select Galatians 6:5

6Mwenye kufundishwa neno la Mungu na amshirikishe mwalimu wake riziki zake.Select Galatians 6:6

7Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.Select Galatians 6:7

8Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uzima wa milele.Select Galatians 6:8

9Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake.Select Galatians 6:9

10Kwa hiyo, tukiwa bado na wakati, tuwatendee watu wote mema, na hasa ndugu wa imani yetu.Select Galatians 6:10

11Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe.Select Galatians 6:11

12Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha ninyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.Select Galatians 6:12

13Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki Sheria; huwataka ninyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.Select Galatians 6:13

14Lakini mimi sitajivunia kamwe chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu.Select Galatians 6:14

15Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; cha maana ni kuwa kiumbe kipya.Select Galatians 6:15

16Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma; amani na huruma kwa Israeli--Wateule wa Mungu.Select Galatians 6:16

17Basi, sasa mtu yeyote asinisumbue tena, maana alama nilizo nazo mwilini mwangu ni zile za Yesu.Select Galatians 6:17

18Ndugu, nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Kristo. Amina.Select Galatians 6:18

Next: Ephesians 1Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Galatians

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.