John 2
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Siku ya tatu kulikuwa na arusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo,Select John 2:1
2naye Yesu alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.Select John 2:2
3Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, "Hawana divai!"Select John 2:3
4Yesu akamjibu, "Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado."Select John 2:4
5Hapo mama yake akawaambia watumishi, "Lolote atakalowaambieni, fanyeni."Select John 2:5
6Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.Select John 2:6
7Yesu akawaambia, "Ijazeni mitungi hiyo maji." Nao wakaijaza mpaka juu.Select John 2:7
8Kisha akawaambia, "Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu."Select John 2:8
9Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi,Select John 2:9
10akamwambia, "Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!"Select John 2:10
11Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonyesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.Select John 2:11
12Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache.Select John 2:12
13Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.Select John 2:13
14Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.Select John 2:14
15Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe wao, akazimwaga sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao.Select John 2:15
16Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, "Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!"Select John 2:16
17Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: "Upendo wangu kwa nyumba yako waniua."Select John 2:17
18Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, "Utafanya muujiza gani kuonyesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?"Select John 2:18
19Yesu akawaambia, "Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu."Select John 2:19
20Hapo Wayahudi wakasema, "Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?"Select John 2:20
21Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya Hekalu ambalo ni mwili wake.Select John 2:21
22Basi, alipofufuliwa kutoka wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno aliyokuwa akisema Yesu.Select John 2:22
23Yesu alipokuwa Yerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka, watu wengi walimwamini walipoona ishara alizozifanya.Select John 2:23
24Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wote.Select John 2:24
25Hakuhitaji kuambiwa chochote juu ya watu, maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni mwao.Select John 2:25
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation