Skip to content
Church.wiki
John

John 4

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane.Select John 4:1

2(Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.)Select John 4:2

3Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya;Select John 4:3

4na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.Select John 4:4

5Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.Select John 4:5

6Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.Select John 4:6

7Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, "Nipatie maji ninywe."Select John 4:7

8(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)Select John 4:8

9Lakini huyo mwanamke akamwambia, "Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?" (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu.)Select John 4:9

10Yesu akamjibu, "Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekwambia: Nipatie maji ninywe, ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yaliyo hai."Select John 4:10

11Huyo mama akasema, "Mheshimiwa, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yaliyo hai?Select John 4:11

12Au, labda wewe wajifanya mkuu kuliko babu yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo yake walikunywa maji ya kisima hiki."Select John 4:12

13Yesu akamjibu, "Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena.Select John 4:13

14Lakini atakayekunywa maji nitakayompa mimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya uzima na kumpatia uzima wa milele."Select John 4:14

15Huyo mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, nipe maji hayo ili nisione kiu tena; nisije tena mpaka hapa kuteka maji."Select John 4:15

16Yesu akamwambia, "Nenda ukamwite mumeo uje naye hapa."Select John 4:16

17Huyo mwanamke akamwambia, "Mimi sina mume." Yesu akamwambia, "Umesema kweli, kwamba huna mume.Select John 4:17

18Maana umekuwa na waume watano, na huyo unayeishi naye sasa si mume wako. Hapo umesema kweli."Select John 4:18

19Huyo Mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, naona ya kuwa wewe u nabii.Select John 4:19

20Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini ninyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudu Mungu ni kule Yerusalemu."Select John 4:20

21Yesu akamwambia, "Niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba juu ya mlima huu, wala kule Yerusalemu.Select John 4:21

22Ninyi Wasamaria mnamwabudu yule msiyemjua, lakini sisi tunamjua huyo tunayemwabudu, kwa maana wokovu unatoka kwa Wayahudi.Select John 4:22

23Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka.Select John 4:23

24Mungu ni Roho, na watu wataweza tu kumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake."Select John 4:24

25Huyo mama akamwambia, "Najua kwamba Masiha, aitwaye Kristo, anakuja. Atakapokuja atatujulisha kila kitu."Select John 4:25

26Yesu akamwambia, "Mimi ninayesema nawe, ndiye."Select John 4:26

27Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: "Unataka nini?" au, "Kwa nini unaongea na mwanamke?"Select John 4:27

28Huyo mama akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu,Select John 4:28

29"Njoni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je, yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?"Select John 4:29

30Watu wakatoka mjini, wakamwendea Yesu.Select John 4:30

31Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwa wanamsihi Yesu: "Mwalimu, ule chakula."Select John 4:31

32Lakini Yesu akawaambia, "Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi."Select John 4:32

33Wanafunzi wake wakaulizana, "Je, kuna mtu aliyemletea chakula?"Select John 4:33

34Yesu akawaambia, "Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.Select John 4:34

35Ninyi mwasema: Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika! Lakini mimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yako tayari kuvunwa.Select John 4:35

36Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja.Select John 4:36

37Kwa sababu hiyo msemo huu ni kweli: Mmoja hupanda na mwingine huvuna.Select John 4:37

38Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho, wengine walifanya kazi, lakini ninyi mnafaidika kutokana na jasho lao."Select John 4:38

39Wasamaria wengi wa kijiji kile waliamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: "Ameniambia mambo yote niliyofanya."Select John 4:39

40Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili.Select John 4:40

41Watu wengi zaidi walimwamini kwa sababu ya ujumbe wake.Select John 4:41

42Wakamwambia yule mama, "Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu."Select John 4:42

43Baada ya siku mbili Yesu aliondoka hapo, akaenda Galilaya.Select John 4:43

44Maana Yesu mwenyewe alisema waziwazi kwamba, "Nabii hapati heshima katika nchi yake."Select John 4:44

45Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.Select John 4:45

46Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.Select John 4:46

47Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.Select John 4:47

48Yesu akamwambia, "Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!"Select John 4:48

49Huyo ofisa akamwambia, "Mheshimiwa, tafadhali twende kabla mwanangu hajafa."Select John 4:49

50Yesu akamwambia, "Nenda tu, mwanao yu mzima." Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.Select John 4:50

51Alipokuwa bado njiani, watumishi wake walikutana naye, wakamwambia kwamba mwanawe alikuwa mzima.Select John 4:51

52Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, "Jana saa saba mchana, homa ilimwacha."Select John 4:52

53Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: "Mwanao yu mzima." Basi, yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote.Select John 4:53

54Hii ilikuwa ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipokuwa anatoka Yudea kwenda Galilaya.Select John 4:54

Next: John 5Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

John

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.