Luke 1
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Mheshimiwa Theofilo: Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu.Select Luke 1:1
2Waliandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo.Select Luke 1:2
3Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango,Select Luke 1:3
4ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa.Select Luke 1:4
5Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.Select Luke 1:5
6Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.Select Luke 1:6
7Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana.Select Luke 1:7
8Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu,Select Luke 1:8
9Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani.Select Luke 1:9
10Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani.Select Luke 1:10
11Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.Select Luke 1:11
12Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.Select Luke 1:12
13Lakini malaika akamwambia, "Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.Select Luke 1:13
14Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake.Select Luke 1:14
15Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.Select Luke 1:15
16Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao.Select Luke 1:16
17Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama Eliya. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake."Select Luke 1:17
18Zakariya akamwambia huyo malaika, "Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu."Select Luke 1:18
19Malaika akamjibu, "Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema.Select Luke 1:19
20Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia."Select Luke 1:20
21Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni.Select Luke 1:21
22Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.Select Luke 1:22
23Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani.Select Luke 1:23
24Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema:Select Luke 1:24
25"Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu."Select Luke 1:25
26Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya,Select Luke 1:26
27kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi.Select Luke 1:27
28Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe."Select Luke 1:28
29Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini?Select Luke 1:29
30Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.Select Luke 1:30
31Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu.Select Luke 1:31
32Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake.Select Luke 1:32
33Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho."Select Luke 1:33
34Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?"Select Luke 1:34
35Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu.Select Luke 1:35
36Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa.Select Luke 1:36
37Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu."Select Luke 1:37
38Maria akasema, "Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema." Kisha yule malaika akaenda zake.Select Luke 1:38
39Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yuda.Select Luke 1:39
40Huko, aliingia katika nyumba ya Zakariya, akamsalimu Elisabeti.Select Luke 1:40
41Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifiu,Select Luke 1:41
42akasema kwa sauti kubwa, "Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa.Select Luke 1:42
43Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?Select Luke 1:43
44Nakwambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.Select Luke 1:44
45Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokwambia."Select Luke 1:45
46Naye Maria akasema,Select Luke 1:46
47"Moyo wangu wamtukuza Bwana, roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.Select Luke 1:47
48Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu. Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.Select Luke 1:48
49Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu, jina lake ni takatifu.Select Luke 1:49
50Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi.Select Luke 1:50
51Amefanya mambo makuu kwa mkono wake: amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;Select Luke 1:51
52amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu.Select Luke 1:52
53Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaacha waende mikono mitupu.Select Luke 1:53
54Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake.Select Luke 1:54
55Kama alivyowaahidia wazee wetu Abrahamu na wazawa wake hata milele."Select Luke 1:55
56Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake.Select Luke 1:56
57Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume.Select Luke 1:57
58Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.Select Luke 1:58
59Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakariya.Select Luke 1:59
60Lakini mama yake akasema, "La, sivyo, bali ataitwa Yohane."Select Luke 1:60
61Wakamwambia, "Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?"Select Luke 1:61
62Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani.Select Luke 1:62
63Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: "Yohane ndilo jina lake." Wote wakastaajabu.Select Luke 1:63
64Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariya vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.Select Luke 1:64
65Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.Select Luke 1:65
66Wote waliosikia mambo hayo waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: "Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?" Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye.Select Luke 1:66
67Zakariya, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka ujumbe wa Mungu:Select Luke 1:67
68"Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli, kwani amekuja kuwasaidia na kuwakomboa watu wake.Select Luke 1:68
69Ametupatia Mwokozi shujaa, mzawa wa Daudi mtumishi wake.Select Luke 1:69
70Aliahidi hapo kale kwa njia ya manabii wake watakatifu,Select Luke 1:70
71kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.Select Luke 1:71
72Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu.Select Luke 1:72
73Kiapo alichomwapia Abrahamu baba yetu, ni kwamba atatujalia sisiSelect Luke 1:73
74tukombolewe kutoka adui zetu, tupate kumtumikia bila hofu,Select Luke 1:74
75kwa unyofu na uadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu.Select Luke 1:75
76Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu, utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;Select Luke 1:76
77kuwatangazia watu kwamba wataokolewa kwa kuondolewa dhambi zao.Select Luke 1:77
78Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma. Atasababisha pambazuko angavu la ukombozi litujie kutoka juu,Select Luke 1:78
79na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo, aongoze hatua zetu katika njia ya amani."Select Luke 1:79
80Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka alipojionyesha rasmi kwa watu wa Israeli.Select Luke 1:80
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation