Luke 17
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.Select Luke 17:1
2Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.Select Luke 17:2
3Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe.Select Luke 17:3
4Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema Nimetubu, lazima umsamehe."Select Luke 17:4
5Mitume wakamwambia Bwana, "Utuongezee imani."Select Luke 17:5
6Naye Bwana akajibu, "Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: Ng'oka ukajipandikize baharini, nao ungewatii.Select Luke 17:6
7"Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: Haraka, njoo ule chakula?Select Luke 17:7
8La! Atamwambia: Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.Select Luke 17:8
9Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa?Select Luke 17:9
10Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya."Select Luke 17:10
11Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa Samaria na Galilaya.Select Luke 17:11
12Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.Select Luke 17:12
13Wakapaza sauti wakisema, "Yesu Mwalimu, tuonee huruma!"Select Luke 17:13
14Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.Select Luke 17:14
15Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.Select Luke 17:15
16Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.Select Luke 17:16
17Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?Select Luke 17:17
18Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?"Select Luke 17:18
19Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako; imani yako imekuponya."Select Luke 17:19
20Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, "Ufalme wa Mungu utakuja lini?" Naye akawajibu, "Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.Select Luke 17:20
21Wala hakuna atakayeweza kusema, Uko hapa, au Uko pale. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu."Select Luke 17:21
22Halafu akawaambia wanafunzi wake, "Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.Select Luke 17:22
23Na watu watawaambieni: Tazameni yuko hapa; ninyi msitoke wala msiwafuate.Select Luke 17:23
24Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.Select Luke 17:24
25Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.Select Luke 17:25
26Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu.Select Luke 17:26
27Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.Select Luke 17:27
28Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.Select Luke 17:28
29Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote.Select Luke 17:29
30Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.Select Luke 17:30
31"Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.Select Luke 17:31
32Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti.Select Luke 17:32
33Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa.Select Luke 17:33
34Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa.Select Luke 17:34
35Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa."Select Luke 17:35
36Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.Select Luke 17:36
37Hapo wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia."Select Luke 17:37
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation