Luke 19
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo.Select Luke 19:1
2Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.Select Luke 19:2
3Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu.Select Luke 19:3
4Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo.Select Luke 19:4
5Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, "Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako."Select Luke 19:5
6Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.Select Luke 19:6
7Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunung'unika wakisema, "Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi."Select Luke 19:7
8Lakini Zakayo akasimama akamwambia Yesu, "Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne."Select Luke 19:8
9Yesu akamwambia, "Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.Select Luke 19:9
10Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea."Select Luke 19:10
11Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. (Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, Ufalme wa Mungu ungefika.)Select Luke 19:11
12Hivyo akawaambia, "Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.Select Luke 19:12
13Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kumwambia: Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.Select Luke 19:13
14Lakini wananchi wenzake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende wakaseme: Hatumtaki huyu atutawale.Select Luke 19:14
15"Huyo mtu mashuhuri alirudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, na mara akaamuru wale watumishi aliowapa zile fedha waitwe ili aweze kujua kila mmoja amepata faida gani.Select Luke 19:15
16Mtumishi wa kwanza akatokea, akasema: Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara kumi ya zile fedha ulizonipa.Select Luke 19:16
17Naye akamwambia: Vema; wewe ni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi!Select Luke 19:17
18Mtumishi wa pili akaja, akasema: Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara tano ya zile fedha ulizonipa.Select Luke 19:18
19Naye akamwambia pia: Nawe utakuwa na madaraka juu ya miji mitano.Select Luke 19:19
20"Mtumishi mwingine akaja, akasema: Chukua fedha yako; niliificha salama katika kitambaa,Select Luke 19:20
21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na huchuma ambacho hukupanda.Select Luke 19:21
22Naye akamwambia: Nakuhukumu kutokana na msemo wako, ewe mtumishi mbaya! Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, ambaye huchukua yasiyo yangu na kuchuma nisichopanda.Select Luke 19:22
23Kwa nini basi, hukuiweka fedha yangu benki, nami ningeichukua pamoja na faida baada ya kurudi kwangu?Select Luke 19:23
24Hapo akawaambia wale waliokuwa pale: Mnyang'anyeni hizo fedha, mkampe yule aliyepata faida mara kumi.Select Luke 19:24
25Nao wakamwambia: Lakini Mheshimiwa, huyo ana faida ya kiasi hicho mara kumi!Select Luke 19:25
26Naye akawajibu: Kila aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.Select Luke 19:26
27Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu."Select Luke 19:27
28Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu.Select Luke 19:28
29Alipokaribia kufika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,Select Luke 19:29
30akawaambia: "Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana punda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamlete hapa.Select Luke 19:30
31Kama mtu akiwauliza, kwa nini mnamfungua, mwambieni, Bwana ana haja naye."Select Luke 19:31
32Basi, wakaenda, wakakuta sawa kama alivyowaambia.Select Luke 19:32
33Walipokuwa wanamfungua yule mwana punda, wenyewe wakawauliza, "Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?"Select Luke 19:33
34Nao wakawajibu, "Bwana anamhitaji."Select Luke 19:34
35Basi, wakampelekea Yesu yule mwana punda. Kisha wakatandika mavazi yao juu yake wakampandisha Yesu.Select Luke 19:35
36Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani.Select Luke 19:36
37Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake, wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;Select Luke 19:37
38wakawa wanasema: "Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!"Select Luke 19:38
39Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu, wakamwambia Yesu, "Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!"Select Luke 19:39
40Yesu akawajibu, "Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti."Select Luke 19:40
41Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliuliliaSelect Luke 19:41
42akisema: "Laiti ungelijua leo hii yale yaletayo amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.Select Luke 19:42
43Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote.Select Luke 19:43
44Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hata jiwe moja juu jingine, kwa sababu hukuutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa."Select Luke 19:44
45Kisha, Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuzia nje wafanyabiasharaSelect Luke 19:45
46akisema, "Imeandikwa: Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi."Select Luke 19:46
47Yesu akawa anafundisha kila siku Hekaluni. Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumwangamiza,Select Luke 19:47
48lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa.Select Luke 19:48
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation