Skip to content
Church.wiki
Luke

Luke 20

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamoja na wazee walifika,Select Luke 20:1

2wakasema, "Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?"Select Luke 20:2

3Yesu akawaambia, "Na mimi nitawaulizeni swali:Select Luke 20:3

4mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?"Select Luke 20:4

5Lakini wao wakajadiliana hivi: "Tukisema yalitoka mbinguni, yeye atatuuliza: Mbona hamkumsadiki?Select Luke 20:5

6Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii."Select Luke 20:6

7Basi, wakamwambia, "Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi."Select Luke 20:7

8Yesu akawaambia, "Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani."Select Luke 20:8

9Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: "Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.Select Luke 20:9

10Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo wakamrudisha mikono mitupu.Select Luke 20:10

11Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.Select Luke 20:11

12Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza.Select Luke 20:12

13Yule mwenye shamba akafikiri: Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi; labda watamjali yeye.Select Luke 20:13

14Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: Huyu ndiye mrithi. Basi, tumwue ili urithi wake uwe wetu.Select Luke 20:14

15Basi, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamwua." Yesu akauliza, "Yule mwenye shamba atawafanya nini hao wakulima?Select Luke 20:15

16Atakuja kuwaangamiza wakulima hao, na atawapa wakulima wengine hilo shamba la mizabibu." Watu waliposikia maneno hayo, walisema: "Hasha! Yasitukie hata kidogo!"Select Luke 20:16

17Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, "Maandiko haya Matakatifu yana maana gani basi? Jiwe walilokataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!Select Luke 20:17

18Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo, atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamsaga kabisa."Select Luke 20:18

19Walimu wa Sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.Select Luke 20:19

20Basi, wakawa wanatafuta wakati wa kufaa. Wakawahonga watu fulani wajisingizie kuwa wema, wakawatuma wamnase Yesu kwa maswali, na hivyo waweze kumtia nguvuni na kumpeleka kwa wakuu wa serikali.Select Luke 20:20

21Hao wapelelezi wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.Select Luke 20:21

22Basi, twambie kama ni halali, au la, kulipa kodi kwa Kaisari!"Select Luke 20:22

23Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,Select Luke 20:23

24"Nionyesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?"Select Luke 20:24

25Nao wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Yesu akawaambia, "Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake Kaisari, na Mungu vilivyo vyake Mungu."Select Luke 20:25

26Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.Select Luke 20:26

27Kisha Masadukayo, ambao husema kwamba wafu hawafufuki, wakamjia Yesu, wakasema:Select Luke 20:27

28"Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, amzalie watoto ndugu yake marehemu.Select Luke 20:28

29Sasa, wakati mmoja kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza alioa na baadaye akafa bila kuacha mtoto.Select Luke 20:29

30Yule ndugu wa pili akamwoa yule mjane, naye pia, akafa;Select Luke 20:30

31na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba--wote walikufa bila kuacha watoto.Select Luke 20:31

32Mwishowe akafa pia yule mwanamke.Select Luke 20:32

33Je, siku wafu watakapofufuliwa, mwanamke huyo atakuwa mke wa nani? Alikuwa ameolewa na wote saba."Select Luke 20:33

34Yesu akawaambia, "Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa;Select Luke 20:34

35lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa.Select Luke 20:35

36Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.Select Luke 20:36

37Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.Select Luke 20:37

38Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana wale aliowaita kwake, wanaishi naye."Select Luke 20:38

39Baadhi ya wale walimu wa Sheria wakasema, "Mwalimu, umejibu vema kabisa."Select Luke 20:39

40Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.Select Luke 20:40

41Yesu akawauliza, "Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?Select Luke 20:41

42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kuliaSelect Luke 20:42

43mpaka niwafanye adui zako kama kiti cha kuwekea miguu yako.Select Luke 20:43

44Ikiwa Daudi anamwita yeye, Bwana, basi atakuwaje mwanawe?"Select Luke 20:44

45Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote,Select Luke 20:45

46"Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.Select Luke 20:46

47Huwadhulumu wajane huku wakisingizia kuwa wema kwa kusali sala ndefu. Hao watapata hukumu kali zaidi!"Select Luke 20:47

Next: Luke 21Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Luke

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.