Skip to content
Church.wiki
Mark

Mark 1

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.Select Mark 1:1

2Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: "Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako.Select Mark 1:2

3Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapito yake."Select Mark 1:3

4Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba ni lazima watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.Select Mark 1:4

5Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.Select Mark 1:5

6Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwa manyoya ya ngamia, na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.Select Mark 1:6

7Naye alihubiri akisema, "Baada yangu anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake.Select Mark 1:7

8Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu."Select Mark 1:8

9Siku hizo, Yesu alifika kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, akabatizwa na Yohane katika mto Yordani.Select Mark 1:9

10Mara tu alipotoka majini, aliona mbingu zimefunguliwa, na Roho akishuka juu yake kama njiwa.Select Mark 1:10

11Sauti ikasikika kutoka mbinguni: "Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe."Select Mark 1:11

12Mara akaongozwa na Roho kwenda jangwani,Select Mark 1:12

13akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamtumikia.Select Mark 1:13

14Yohane alipokwisha fungwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya, akahubiri Habari Njema ya Mungu, akisema,Select Mark 1:14

15"Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!"Select Mark 1:15

16Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.Select Mark 1:16

17Yesu akawaambia, "Nifuateni nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."Select Mark 1:17

18Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.Select Mark 1:18

19Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Nao pia walikuwa ndani ya mashua yao wakizitengeneza nyavu zao.Select Mark 1:19

20Yesu akawaita mara, nao wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua pamoja na wafanyakazi, wakamfuata.Select Mark 1:20

21Wakafika mjini Kafarnaumu, na mara ilipofika Sabato, Yesu akaingia katika Sunagogi, akaanza kufundisha.Select Mark 1:21

22Watu wote waliomsikia walishangazwa na mafundisho yake, maana hakuwa anafundisha kama walimu wao wa Sheria, bali kama mtu mwenye mamlaka.Select Mark 1:22

23Mara akatokea mle ndani ya sunagogi mtu mmoja mwenye pepo mchafu,Select Mark 1:23

24akapaaza sauti, "Una nini nasi, wewe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!"Select Mark 1:24

25Yesu akamkemea, "Nyamaza! Mtoke mtu huyu."Select Mark 1:25

26Basi, huyo pepo mchafu akamtikisatikisa mtu huyo, kisha akalia kwa sauti kubwa, akamtoka.Select Mark 1:26

27Watu wote wakashangaa, wakaulizana, "Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!"Select Mark 1:27

28Habari za Yesu zikaenea upesi kila mahali katika wilaya ya Galilaya.Select Mark 1:28

29Wakatoka katika sunagogi, wakaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea; Yakobo na Yohane walikwenda pamoja nao.Select Mark 1:29

30Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.Select Mark 1:30

31Yesu akamwendea huyo mama, akamshika mkono, akamwinua. Na ile homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.Select Mark 1:31

32Jioni, jua lilipokwisha tua, wakamletea Yesu wagonjwa wote na watu waliopagawa na pepo.Select Mark 1:32

33Watu wote wa mji ule wakakusanyika nje ya mlango.Select Mark 1:33

34Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.Select Mark 1:34

35Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali.Select Mark 1:35

36Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta.Select Mark 1:36

37Walipomwona wakamwambia, "Kila mtu anakutafuta."Select Mark 1:37

38Yesu akawaambia, "Twendeni katika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maana nimekuja kwa sababu hiyo."Select Mark 1:38

39Basi, akaenda kila mahali Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo.Select Mark 1:39

40Mtu mmoja mwenye ukoma alimwendea Yesu, akapiga magoti, akamwomba, "Ukitaka, waweza kunitakasa!"Select Mark 1:40

41Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, "Nataka, takasika!"Select Mark 1:41

42Mara ukoma ukamwacha mtu huyo, akatakasika.Select Mark 1:42

43Kisha Yesu akamwambia aende zake upesi na kumwonya vikali,Select Mark 1:43

44"Usimwambie mtu yeyote jambo hili, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani; kisha utoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona."Select Mark 1:44

45Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.Select Mark 1:45

Next: Mark 2Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Mark

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.