Skip to content
Church.wiki
Mark

Mark 13

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, "Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!"Select Mark 13:1

2Yesu akamwambia, "Je, unayaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitabomolewa."Select Mark 13:2

3Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwa faragha,Select Mark 13:3

4"Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?"Select Mark 13:4

5Yesu akaanza kuwaambia, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.Select Mark 13:5

6Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.Select Mark 13:6

7Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.Select Mark 13:7

8Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.Select Mark 13:8

9"Lakini ninyi jihadharini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, na kuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kunishuhudia kwao.Select Mark 13:9

10Lakini lazima kwanza Habari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote.Select Mark 13:10

11Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.Select Mark 13:11

12Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.Select Mark 13:12

13Watu wote watawachukieni ninyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.Select Mark 13:13

14"Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.Select Mark 13:14

15Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu.Select Mark 13:15

16Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.Select Mark 13:16

17Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!Select Mark 13:17

18Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.Select Mark 13:18

19Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.Select Mark 13:19

20Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.Select Mark 13:20

21"Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki.Select Mark 13:21

22Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana.Select Mark 13:22

23Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea.Select Mark 13:23

24"Basi, siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.Select Mark 13:24

25Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.Select Mark 13:25

26Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.Select Mark 13:26

27Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.Select Mark 13:27

28"Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.Select Mark 13:28

29Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana.Select Mark 13:29

30Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.Select Mark 13:30

31Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.Select Mark 13:31

32"Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.Select Mark 13:32

33Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.Select Mark 13:33

34Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.Select Mark 13:34

35Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.Select Mark 13:35

36Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.Select Mark 13:36

37Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!"Select Mark 13:37

Next: Mark 14Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Mark

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.