Mark 15
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.Select Mark 15:1
2Pilato akamwuliza Yesu, "Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu akajibu, "Wewe umesema."Select Mark 15:2
3Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi.Select Mark 15:3
4Pilato akamwuliza tena Yesu, "Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako."Select Mark 15:4
5Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa.Select Mark 15:5
6Kila wakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturi ya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka.Select Mark 15:6
7Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.Select Mark 15:7
8Watu wengi wakamwendea Pilato wakamwomba awafanyie kama kawaida yake.Select Mark 15:8
9Pilato akawauliza, "Je, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?"Select Mark 15:9
10Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.Select Mark 15:10
11Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.Select Mark 15:11
12Pilato akawauliza tena, "Basi, sasa mwataka nifanye nini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?"Select Mark 15:12
13Watu wote wakapaaza sauti tena: "Msulubishe!"Select Mark 15:13
14Lakini Pilato akawauliza, "Kwa nini! Amefanya kosa gani?" Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, "Msulubishe!"Select Mark 15:14
15Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.Select Mark 15:15
16Kisha askari walimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakakusanya kikosi kizima cha askari.Select Mark 15:16
17Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekea kichwani.Select Mark 15:17
18Wakaanza kumsalimu, "Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!"Select Mark 15:18
19Wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsujudia.Select Mark 15:19
20Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.Select Mark 15:20
21Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.Select Mark 15:21
22Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la Kichwa."Select Mark 15:22
23Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini yeye akaikataa.Select Mark 15:23
24Basi, wakamsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamue nani angepata nini.Select Mark 15:24
25Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha.Select Mark 15:25
26Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa: "Mfalme wa Wayahudi."Select Mark 15:26
27Pamoja naye waliwasulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.Select Mark 15:27
28Hapo yakatimia Maandiko Matakatifu yanayosema, "Aliwekwa kundi moja na waovu."Select Mark 15:28
29Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao na kusema, "Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu!Select Mark 15:29
30Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!"Select Mark 15:30
31Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, "Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!Select Mark 15:31
32Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini." Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.Select Mark 15:32
33Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.Select Mark 15:33
34Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eloi, Eloi, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"Select Mark 15:34
35Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo, walisema, "Sikiliza! Anamwita Eliya!"Select Mark 15:35
36Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, "Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!"Select Mark 15:36
37Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.Select Mark 15:37
38Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini.Select Mark 15:38
39Jemadari mmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsi Yesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, "Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!"Select Mark 15:39
40Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.Select Mark 15:40
41Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa na wanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye.Select Mark 15:41
42Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyo ilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotangulia Sabato.Select Mark 15:42
43Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.Select Mark 15:43
44Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesu alikuwa amekufa kitambo.Select Mark 15:44
45Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.Select Mark 15:45
46Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.Select Mark 15:46
47Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.Select Mark 15:47
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation