Matthew 23
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake,Select Matthew 23:1
2"Walimu wa Sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua Sheria ya Mose.Select Matthew 23:2
3Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.Select Matthew 23:3
4Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.Select Matthew 23:4
5Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.Select Matthew 23:5
6Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika masunagogi.Select Matthew 23:6
7Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na watu: Mwalimu.Select Matthew 23:7
8Lakini ninyi msiitwe kamwe Mwalimu, maana mwalimu wenu ni mmoja tu, nanyi nyote ni ndugu.Select Matthew 23:8
9Wala msimwite mtu yeyote Baba hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu aliye mbinguni.Select Matthew 23:9
10Wala msiitwe Viongozi, maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo.Select Matthew 23:10
11Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.Select Matthew 23:11
12Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.Select Matthew 23:12
13"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.Select Matthew 23:13
14Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.Select Matthew 23:14
15"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe.Select Matthew 23:15
16"Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, kiapo hicho kinamshika.Select Matthew 23:16
17Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu au Hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu?Select Matthew 23:17
18Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.Select Matthew 23:18
19Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, au madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu?Select Matthew 23:19
20Anayeapa kwa madhabahu ameapa kwa hiyo madhabahu, na kwa chochote kilichowekwa juu yake.Select Matthew 23:20
21Na anayeapa kwa Hekalu ameapa kwa hilo Hekalu na pia kwa yule akaaye ndani yake.Select Matthew 23:21
22Na anayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa huyo aketiye juu yake.Select Matthew 23:22
23Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.Select Matthew 23:23
24Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!Select Matthew 23:24
25"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.Select Matthew 23:25
26Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.Select Matthew 23:26
27"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.Select Matthew 23:27
28Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.Select Matthew 23:28
29"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.Select Matthew 23:29
30Mwasema: Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii!Select Matthew 23:30
31Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu waliowaua manabii.Select Matthew 23:31
32Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza!Select Matthew 23:32
33Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?Select Matthew 23:33
34Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.Select Matthew 23:34
35Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.Select Matthew 23:35
36Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya mambo haya.Select Matthew 23:36
37"Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.Select Matthew 23:37
38Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame.Select Matthew 23:38
39Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana."Select Matthew 23:39
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation