Skip to content
Church.wiki
Matthew

Matthew 27

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.Select Matthew 27:1

2Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.Select Matthew 27:2

3Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu thelathini za fedha.Select Matthew 27:3

4Akawaambia, "Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe." Lakini wao wakasema, "Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako."Select Matthew 27:4

5Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga.Select Matthew 27:5

6Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, "Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu."Select Matthew 27:6

7Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.Select Matthew 27:7

8Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.Select Matthew 27:8

9Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: "Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga bei,Select Matthew 27:9

10wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza."Select Matthew 27:10

11Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, "Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamwambia, "Wewe umesema."Select Matthew 27:11

12Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno.Select Matthew 27:12

13Hivyo Pilato akamwuliza, "Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?"Select Matthew 27:13

14Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana.Select Matthew 27:14

15Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka.Select Matthew 27:15

16Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba.Select Matthew 27:16

17Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, "Mwataka nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Baraba ama Yesu aitwae Kristo?"Select Matthew 27:17

18Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu.Select Matthew 27:18

19Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake akampelekea ujumbe: "Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake."Select Matthew 27:19

20Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe.Select Matthew 27:20

21Mkuu wa mkoa akawauliza, "Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?" Wakamjibu, "Baraba!"Select Matthew 27:21

22Pilato akawauliza, "Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?" Wote wakasema, "Asulubiwe!"Select Matthew 27:22

23Pilato akauliza, "Kwa nini? Amefanya kosa gani?" Wao wakazidi kupaaza sauti: "Asulubiwe!"Select Matthew 27:23

24Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, "Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe."Select Matthew 27:24

25Watu wote wakasema, "Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!"Select Matthew 27:25

26Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa Yesu asulubiwe.Select Matthew 27:26

27Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima.Select Matthew 27:27

28Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.Select Matthew 27:28

29Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, "Shikamoo mfalme wa Wayahudi!"Select Matthew 27:29

30Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.Select Matthew 27:30

31Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.Select Matthew 27:31

32Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.Select Matthew 27:32

33Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la kichwa,"Select Matthew 27:33

34wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.Select Matthew 27:34

35Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.Select Matthew 27:35

36Wakaketi, wakawa wanamchunga.Select Matthew 27:36

37Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi."Select Matthew 27:37

38Wanyang'anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.Select Matthew 27:38

39Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema,Select Matthew 27:39

40"Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!"Select Matthew 27:40

41Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na wazee walimdhihaki wakisema,Select Matthew 27:41

42"Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.Select Matthew 27:42

43Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka."Select Matthew 27:43

44Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana.Select Matthew 27:44

45Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza.Select Matthew 27:45

46Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eli, Eli, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"Select Matthew 27:46

47Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema, "Anamwita Eliya."Select Matthew 27:47

48Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe.Select Matthew 27:48

49Wengine wakasema, "Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa."Select Matthew 27:49

50Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho.Select Matthew 27:50

51Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;Select Matthew 27:51

52makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa;Select Matthew 27:52

53nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi.Select Matthew 27:53

54Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, "Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu."Select Matthew 27:54

55Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia.Select Matthew 27:55

56Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo.Select Matthew 27:56

57Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.Select Matthew 27:57

58Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe.Select Matthew 27:58

59Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani,Select Matthew 27:59

60akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.Select Matthew 27:60

61Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi kulielekea kaburi.Select Matthew 27:61

62Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato,Select Matthew 27:62

63Wakasema, "Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, Baada ya siku tatu nitafufuka.Select Matthew 27:63

64Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali."Select Matthew 27:64

65Pilato akawaambia, "Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri mjuavyo."Select Matthew 27:65

66Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile jiwe na kuacha hapo askari walinzi.Select Matthew 27:66

Next: Matthew 28Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Matthew

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.