Skip to content
Church.wiki
Matthew

Matthew 4

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.Select Matthew 4:1

2Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.Select Matthew 4:2

3Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate."Select Matthew 4:3

4Yesu akamjibu, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu."Select Matthew 4:4

5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,Select Matthew 4:5

6akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe."Select Matthew 4:6

7Yesu akamwambia, "Imeandikwa pia: Usimjaribu Bwana, Mungu wako."Select Matthew 4:7

8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,Select Matthew 4:8

9akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu."Select Matthew 4:9

10Hapo, Yesu akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake."Select Matthew 4:10

11Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.Select Matthew 4:11

12Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.Select Matthew 4:12

13Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.Select Matthew 4:13

14Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:Select Matthew 4:14

15"Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng'ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!Select Matthew 4:15

16Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!"Select Matthew 4:16

17Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, "Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!"Select Matthew 4:17

18Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.Select Matthew 4:18

19Basi, akawaambia, "Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."Select Matthew 4:19

20Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.Select Matthew 4:20

21Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita,Select Matthew 4:21

22nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.Select Matthew 4:22

23Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.Select Matthew 4:23

24Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.Select Matthew 4:24

25Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng'ambo ya mto Yordani, walimfuata.Select Matthew 4:25

Next: Matthew 5Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Matthew

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.