Skip to content
Church.wiki
Matthew

Matthew 5

Swahili

Translation: SWAHILI

Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources

Start reading

1Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,Select Matthew 5:1

2naye akaanza kuwafundisha:Select Matthew 5:2

3"Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.Select Matthew 5:3

4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.Select Matthew 5:4

5Heri walio wapole, maana watairithi nchi.Select Matthew 5:5

6Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.Select Matthew 5:6

7Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.Select Matthew 5:7

8Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.Select Matthew 5:8

9Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.Select Matthew 5:9

10Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.Select Matthew 5:10

11"Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.Select Matthew 5:11

12Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.Select Matthew 5:12

13"Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.Select Matthew 5:13

14"Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.Select Matthew 5:14

15Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.Select Matthew 5:15

16Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni."Select Matthew 5:16

17"Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.Select Matthew 5:17

18Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.Select Matthew 5:18

19Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.Select Matthew 5:19

20Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.Select Matthew 5:20

21"Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.Select Matthew 5:21

22Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: Pumbavu atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.Select Matthew 5:22

23Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,Select Matthew 5:23

24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.Select Matthew 5:24

25"Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.Select Matthew 5:25

26Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya mwisho.Select Matthew 5:26

27"Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!Select Matthew 5:27

28Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.Select Matthew 5:28

29Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling'oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.Select Matthew 5:29

30Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.Select Matthew 5:30

31"Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.Select Matthew 5:31

32Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.Select Matthew 5:32

33"Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.Select Matthew 5:33

34Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu;Select Matthew 5:34

35wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.Select Matthew 5:35

36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.Select Matthew 5:36

37Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.Select Matthew 5:37

38"Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino.Select Matthew 5:38

39Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.Select Matthew 5:39

40Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.Select Matthew 5:40

41Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.Select Matthew 5:41

42Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopa kitu usimnyime.Select Matthew 5:42

43"Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.Select Matthew 5:43

44Lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyiSelect Matthew 5:44

45ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.Select Matthew 5:45

46Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi? Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!Select Matthew 5:46

47Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.Select Matthew 5:47

48Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.Select Matthew 5:48

Next: Matthew 6Continue reading

Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation

Reading settings

Choose a passage

Old Testament

New Testament

Matthew

Selected verses

Select another verse to extend the range.

Highlight

My Bible

About this name

Listen

Uses an English voice provided by your browser.