Philemon 1
Swahili
Translation: SWAHILI
Modern translations such as the NIV or ESV are not available yet. They need a license, and we will add them when one is in place. All translations and their sources
1Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo, ninakuandikia wewe Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetuSelect Philemon 1:1
2na kanisa linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na askari mwenzetu Arkupo.Select Philemon 1:2
3Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana yesu Kristo.Select Philemon 1:3
4Kila wakati ninaposali nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru MunguSelect Philemon 1:4
5maana nasikia habari za imani yako kwa Bwana wetu Yesu na upendo wako kwa watu wote wa Mungu.Select Philemon 1:5
6Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.Select Philemon 1:6
7Ndugu, upendo wako yameniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.Select Philemon 1:7
8Kwa sababu hiyo, ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa ndugu yako katika Kristo, kukuamuru ufanye unachopaswa kufanya.Select Philemon 1:8
9Lakini kwa sababu ya upendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanya hivi ingawa mimi ni Paulo, balozi wa Kristo Yesu, na sasa pia mfungwa kwa ajili yake.Select Philemon 1:9
10Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.Select Philemon 1:10
11Ni Onesimo yuleyule ambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu, lakini sasa ananifaa mimi na wewe pia.Select Philemon 1:11
12Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe.Select Philemon 1:12
13Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Habari Njema.Select Philemon 1:13
14Lakini sitafanya chochote bila kibali chako. Sipendi kukulazimisha unisaidie, kwani wema wako unapaswa kutokana na hiari yako wewe mwenyewe na si kwa kulazimika.Select Philemon 1:14
15Labda Onesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu, kusudi uweze tena kuwa naye daima.Select Philemon 1:15
16Na sasa yeye si mtumwa tu, ila ni bora zaidi ya mtumwa: yeye ni ndugu yetu mpenzi. Na wa maana sana kwangu mimi, na kwako atakuwa wa maana zaidi kama mtumwa na kama ndugu katika Bwana.Select Philemon 1:16
17Basi, ikiwa wanitambua mimi kuwa mwenzako, mpokee tena kama vile ungenipokea mimi mwenyewe.Select Philemon 1:17
18Kama alikuwa amekukosea kitu, au alikuwa na deni lako, basi, unidai mimi.Select Philemon 1:18
19Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: Mimi Paulo nitalipa! (Tena sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi yako.)Select Philemon 1:19
20Haya, basi, ndugu yangu, nifanyie jambo hilo kwa ajili ya jina la Bwana; burudisha moyo wangu kama ndugu katika Kristo.Select Philemon 1:20
21Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.Select Philemon 1:21
22Pamoja na hayo, nitayarishie chumba kwani natumaini kwamba kwa sala zenu, Mungu atanijalia niwatembeleeni.Select Philemon 1:22
23Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu, anakusalimu.Select Philemon 1:23
24Nao akina Marko, Aristarko, Dema na Luka, wafanyakazi wenzangu, wanakusalimu.Select Philemon 1:24
25Nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.Select Philemon 1:25
Swahili (SWAHILI). Public domain. Text from the CrossWire Bible Society module. About this translation